Chama cha National League for Democracy (NLD)
Chama cha National League for Democracy (NLD) kinapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote waliokijitokeza kwa wingi katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Visiwani kwa ajili ya kumdhamini Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu.
Zoezi la upatikanaji wa wadhamini lilianza rasmi tarehe 10 Agosti 2025, mara baada ya Mheshimiwa Doyo Hassan Doyo, Mgombea wa Urais kupitia NLD, kuchukua fomu ya uteuzi. Zoezi hili limehitimishwa rasmi leo, tarehe 22 Agosti 2025, katika Mkoa wa Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa Lamada, na kufuatiwa na kiapo cha Mgombea huyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, hatua muhimu inayomwezesha sasa kukidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa uteuzi.
Mgombea wetu anatarajia kurudisha fomu ya uteuzi rasmi tarehe 24 Agosti 2025, jijini Dodoma, na kisha kusubiri uamuzi na uteuzi rasmi kutoka Tume Huru ya Uchaguzi.
Tunatambua kwa dhati na kuthamini moyo wa uzalendo, mshikamano na imani mliyoonesha katika hatua hii muhimu ya kisiasa kwa chama chetu na kwa taifa kwa ujumla. NLD itaendelea kusimama imara kwa ajili ya maslahi ya wananchi na maendeleo ya kweli ya Tanzania.
NLD – Ukombozi wa Umma
NLD – Mtetezi wa Umma
Imetolewa na.
Don Waziri Mnyamani
Mkurugezi wa Mipango na Uchaguzi Taifa, NLD
Asanteni.
0 Comments