Na mwandishi wetu
LEO Agosti 21 .2025 Umoja wa Ngome ya Mama ambao unapatikana Kawe Jijini Dar es Salaam umetangaza Kongamano kubwa la Matumizi ya Nishati Safi Kusapoti jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani
Mlezi wa Ngome hiyo Bi Zainab Athumani wakati anazungumza mbele ya Waandishi wa Habari Wakati wa Uzinduzi huo amesema moja ya malengo waliyokua nayo ni Kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ambapo wanataka kwenda Kumsapoti Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani na kupitia njia ya Kongamano ndo alama kubwa ya kuunga mkono jitihada hizo
"Tunataka kumsapoti Mama Dkt.Samia Sulubu Hassaani katika kumuunga mkono tunataka kufanya Kongamano tarehe 26 Mwezi wa 08 Msasani Beach.......
Kongamano litaanza kuzinduliwa katika wilaya ya Kinondoni kata ya Kawe na wamealikwa washindani ambao watashindanishwa ambao ni wakina Mama zaidi ya 20 katika wilaya
Wilaya ya Kinondoni ina kata 20 na kila kata itapeleka mkali wao wa kupika pia
ndani ya Kongamano zitatolewa Elimu ,Kongamano litafanyika karibia Mkoa wote wa Dsm kama ilivyoelezwa na kamati
Aidha Umoja huo una akina Mama /Wanachama zaidi ya 400 na unawakaribisha wadau mbalimbali kuungana nao ili waunge mkono jitihada za matumizi ya nishati safi kwa pamoja
0 Comments