RAIS MWINYI: SMZ ITAENDELEA KULETA MAGEUZI KATIKA MAHKAMA

 



Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuungamkono juhudi za Muhimili wa Mahkama zenye lengo la kuleta mageuzi makubwa katika miundombinu ya majengo ya Mahkama.

Rais Dk.Mwinyi  ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mahkama ya Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ameeleza, Serikali imefanikiwa kuleta mageuzi makubwa kwenye majengo ya Mahkama kwa kutoa fedha za ndani kwa asilimia mia jambo alilolieleza kuwa la kujivunia.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema mageuzi hayo yana lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi katika mazingira yakuridhisha hatua aliyoielezea kwamba itaijengea heshima muhimili huo.

“Tumetumia fedha zetu wenyewe kwasababu tungetumia wafadhili tungechelewa kufikia mafanikio haya” alibainisha Rais Dk. Mwinyi.

Akilizungumzia jengo la zamani la Mahkama ya Vuga, Rais Dk. Mwinyi ameeleza litaendelea kuwa la Mahkama na kuridhia azma ya Mahkama ya kulifanya jengo hilo kuwa makumbusho ya Mahkama.













Post a Comment

0 Comments