Na mwandishi wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema matumizi ya Vifaa vya TEHAMA katika Shule za Sekondari ni pamoja na Kuimarisha ushiriki wa wanafunzi katika kujifunza katika muda wa ziada katika maandalizi ya mitihani yao.
Akizungumza leo Desemba 18, 2024 kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa Shule za Sekondari nchini iliyofanyika katika Shule Maalum ya Wasichana ya Sayansi ya Mkoa wa Dar es salaam iliyopo Manispaa ya Ubungo, Mhe. Mchengerwa amesema vifaa hivyo vinalenga kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa njia ya kisasa kwa kutumia na kujifunza TEHAMA ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia Duniani.
Ameongeza kuwa Vifaa vya TEHAMA vinawezedhabKuandaa mazingira vutivu kwa wanafunzi katika kujifunza masomo mbalimbali hususani wanafunzi wenye mlengo wa kuwa wataalamu wa TEHAMA pamoja na Kutoa nafasi kwa wanafunzi na walimu kupata maarifa na stadi za ziada katika masomo mbalimbaliyatakayowawesha kuimarisha maarifa,
Pia aliongeza kuwa Vifaa hivi vitawezeesha Wanafunzi kupata na kuimarisha stadi za kidigitali (Digital literacy) na Kuwawezesha walimu wa Shule za Sekondari kupata maarifa na stadi za ziada za ufundishaji ikiwemo ufundishaji kwa vitendo na video mbalimbali za matukio ya kimasomo.
Mwisho alisema vifaa vya TEHAMA vitawezesha kufanyika kwa vipindi mbalimbali mtandaoni bila kukutanisha wanafunzi na walimu wao na Kupunguza gharama za uandaaji wa nyezo za kujifunzia na kufundishia ikiwemo urahisi wa kupata matini na vitabu mtandaoni na kuchapa nukuu za masomo katika mazingira ya shule.
0 Comments