Na mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima anakabiliwa na tuhuma nzito za kuwa na familia nje ya utumishi wa Kanisa Katoliki. Licha ya kwamba inajulikana wazi kuwa Padri wa Kanisa Katoliki hapaswi kukiuka masharti ya useja ikiwemo kutokuoa wala kuzaa mtoto lakini kwa Padri Kitima ni tofauti.
Vyanzo vyetu vimechunguza na kubaini kuwa Padri Kitima ana familia, anayohusiana nayo kwa usiri mkubwa ikiwa ni pamoja na mke na mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kama Cyrill Thomas, mwenye umri wa miaka 12. Mtoto huyu inasemekana ni matunda ya uhusiano wake na Honoratha Mhando, ambaye ni mhasibu wa TEC.
Taarifa zinaonyesha kuwa Honoratha Mhando ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Mwanza, na inaelezwa kuwa mahusiano yake na Padri Kitima yalianza muda mrefu wakati kiongozi huyo wa dini alipokuwa anafanya kazi kama Makamu Mkuu wa Chuo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu, Padri Kitima ameonyesha kujali sana familia yake. Ameijengea makazi katika maeneo ya Mbagala, ambako inasemekana Honoratha na mtoto wao wanaishi. Majirani wa nyumba hiyo wanasema wanajua mwanamke huyo ana mume lakini hawajawahi kumuona naye kwa ukaribu kutokana na usiri uliopo.
Hata hivyo, imebainika kwamba taarifa hizi zinajulikana na watu wengi wanaofanya kazi na Padri Kitima pamoja na mzazi mwenzake, Honoratha ambaye ni Mhasibu wa TEC.
Hili linaibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji wa viongozi wa Kanisa Katoliki katika kuheshimu viapo vya useja na kuonyesha mfano bora wa maisha ya kiroho kwa waumini wao.
Ikiwa madai haya ni ya kweli, yanasababisha athari kubwa kwa hadhi ya Kanisa Katoliki na uongozi wa TEC. Hii ni changamoto kwa kanisa kushughulikia masuala ya kiroho na maadili ya viongozi wake kwa uwazi na haki, ili kuendelea kujenga imani na heshima kwa waumini wake. Mashirika ya kidini yanapaswa kuimarisha mfumo wa uwajibikaji, kuhakikisha kuwa viapo vya kiroho na maadili havikiukwi.
0 Comments