RAIS DKT MWINYI AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA 61 YA ZANZIBAR

 




Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika Uwanja wa Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba kushiriki kilele cha Sherehe za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 2025.

Rais Dk.Mwinyi amepokea Salamu ya Rais na kupigwa Mizinga 21 pia amekagua Gwaride maalum la Maadhimisho hayo.

Aidha , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameshiriki Maadhimisho hayo, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali kitaifa kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao nchini,  Vyombo vya Ulinzi na Usalama,  Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa na Wananchi kutoka Mikoa ya Unguja na Pemba.






Post a Comment

0 Comments