Na mwandishi wetu
Chama cha National League for Democracy (NLD) kinapenda kuwataarifu wanachama wake, wapenzi wa demokrasia na wananchi wote kwa ujumla kuwa, baada ya mchakato wa ndani wa chama kukamilika kwa mafanikio, Chama kimewapitisha rasmi wagombea wake wa nafasi za juu katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025.
Kwa heshima kubwa, tunatangaza kwamba
Mhe. Doyo Hassan Doyo ameteuliwa rasmi kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NLD.
Mhe. Mfaume Khamis ameteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama chetu.
Uamuzi huu umetokana na vikao halali vya chama, kufuata taratibu zote za kikatiba, na mapendekezo ya wajumbe wa mkutano mkuu kutoka sehemu mbalimbali kote nchini.
Tuna imani kubwa kwamba viongozi hawa ni mfano wa uongozi bora, wenye maono makubwa ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Watanzania wote. Chama cha NLD kimejizatiti kuendeleza misingi ya demokrasia, Uzalendo, haki, na maendeleo jumuishi kwa kila Mtanzania.
Tunaomba ushirikiano wa wanachama, wapenzi wa chama, na wananchi wote katika safari hii ya matumaini na mabadiliko.
NLD - Mkombozi wa Umma
NLD - Mtetezi wa Umma.
Imetolewa na.
Idara ya Habari na Mawasiliano
Chama cha NLD
Tarehe 10-04-2025
0 Comments