DKT. BITEKO AWASILISHA BUNGENI BAJETI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2025/2026

 




Na mwandishi wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ya kiasi cha shilingi Trilioni 2.2 ambapo asilimia 96.5 ya Bajeti yote ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo  na asilimia 3.5 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. 

Akiwasilisha Bajeti hiyo tarehe 28 Aprili, 2025 bungeni jijini Dodoma, Dkt.Biteko ametaja vipaumbele mbalimbali vya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ikiwemo kuendelea kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, pamoja na kufikisha Gridi ya Taifa katika mikoa iliyosalia ya Rukwa, Kagera, Lindi na Mtwara. 

“ Mhe. Spika, kipaumbele kingine ni kuendelea na usambazaji wa nishati katika vitongoji, maeneo ya migodi, kilimo, viwanda na pampu za maji pamoja na vituo vya afya ili kuwezesha shughuli za uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.” Ameeleza Dkt.Biteko

Post a Comment

0 Comments