Habari na Rahim rai
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Jumanne Muliro ameungana na Askari pamoja na familia zao katika kusherehekea Siku ya familia ya polisi (Police Family Day) iliyofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga vilivyopo Temeke Dar Es salaam Aprili 04,2025.
Kamanda Muliro amesema siku hiyo ni muhimu kwao Polisi kufurahi na familia zao na wananchi kwa pamoja kwani licha ya kua na mambo mengi lakini familia ni nguzo imara inayochangia ufanisi mzuri kwa Askari wawapo kazini.
Kamanda Muliro ametumia wasaha huo pia kuwaambia wakazi wa Temeke na maeneo jirani walio kusanyika katika sherehe hiyo kua Jeshi la Polisi linaendelea kujipanga ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na utulivu mkubwa.
Pia wananchi mbalimbali walijumuika kwenye sherehe hiyo ambayo ilipambwa na Michezo pamoja na burudani nyingi kama vile Mpira wa miguu, kukimbiza kuku, mbio za magunia, Ngoma za asili, sanaa ya maigizo na michezo mingine.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Kungu John Malulu ambae ndie alikua mwenyeji wa Sherehe hiyo amemshukuru Kamanda Muliro kwa niaba ya Askari wote, familia zao na wananchi kwa ujumla kwa ushiriki wake na ameahidi kuendelea kushirikiana na jamii ili Polisi Temeke iendelee kua salama.
0 Comments