RAIS DKT SAMIA AWEKA REKODI BARANI AFRIKA KUHUTUBIA BUNGE LA ANGOLA

 




Na mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kung’ara katika jukwaa la kimataifa kwa kuanza ziara ya kihistoria ya siku tatu nchini Angola, kuanzia Aprili 7 hadi Aprili 9, kwa mwaliko rasmi wa Rais wa Angola, Mhe. João Lourenço.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni sura mpya ya uhusiano wa kidiplomasia barani Afrika, Rais Samia ameweka historia kwa kuwa kiongozi wa kwanza Mwanamke kutoka Afrika kuhutubia Bunge la Angola, tukio lililopokelewa kwa heshima kubwa na kushangiliwa kwa sauti kubwa na wabunge wa Angola.

Ziara hii ni ishara ya mafanikio makubwa ya sera ya Rais Samia ya kidiplomasia ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, hususan ndani ya bara la Afrika. Akiwa na ajenda nzito ya maendeleo na ushirikiano, Rais Samia amepanga kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na mwenyeji wake, Mhe. Lourenço, yakilenga maeneo ya nishati, madini, miundombinu, afya, elimu na utalii.






Post a Comment

0 Comments