RAIS MWINYI AWASILI UINGEREZA

 


Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili Jijini London,  nchini Uingereza tarehe 6 Aprili 2025.

Katika uwanja wa ndege wa London Heathrow, Rais Dkt.Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Mbelwa Kairuki.

Rais Dkt.Mwinyi ataanza ziara yake ya kikazi nchini humo leo na kumaliza tarehe 9 Aprili 2025.




Post a Comment

0 Comments