Na mwandishi wetu
Watu Saba wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa baada ya basi kampuni ya Mvungi kupinduka katika kijiji cha Mamba Msangeni waliyani Mwanga Mkoani Kilimanjaro liliokuwa likitokea Ugweno kwenda Jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 12 asubuhi April 3,2025.
Maigwa amesema basi hilo lenye namba za T 222 DNL liliacha barabara na kupinduka kwenye bonde na kusababisha vifo vya watu 7. Waliokufa ni pamoja na wanaume 2 wanawake 4 na mtoto wa miaka miwili.
"Majeruhi wote wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa ya Mawenzi na ya rufaa ya kikanda ya KCMC pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Mwanga"
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kulimudu gari wakati anapishana na gari lingine kwenye kona kali na kuacha barabara na kutumbukia bondeni.
Amewataja waliofariki kuwa ni Ashura Omary(47) Zaituni Ashimu (52) Halima Omary (2)Judith Mwanga(43) na mtu mmoja iliyatambulika kwa jina moja Bernadeta (20) Haji Abubakari(50) Amadi Mshana (64).
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kusubiri uchunguzi na taarifa nyingine . Dereva wa basi hilo anashikiliwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
0 Comments