DKT. FLORENCE SAMIZI ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENYEKITI KAWAIDA KIGOMA

 


Na mwandishi wetu

Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoa wa Kigoma, Mhe. Dkt. Florence George Samizi ameshiriki mapokezi na ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) ambaye amepokelewa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Kasangezi, Kasulu Mkoani Kigoma Jumapili 22 Juni, 2025.

Mwenyekiti Kawaida amewasili Kigoma kwa ajili ya kufunga Semina ya Mafunzo kwa Vijana wa CCM katika Mkoa huo.

Mhe. Dkt. Florence George Samizi ameambatana na Mwenyekiti Kawaida pamoja na viongozi wengine kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo wameridhishwa sana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 

Vilevile, Mwenyekiti Kawaida amemkabidhi Mhe. Dkt. Florence George Samizi Cheti cha shukrani kwa kuchangia shughuli za kambi ya vijana ya iliyohitimishwa tarehe 22 Juni, 2025.


Vijana Tunasema 

OKTOBA TUNATIKI ✅✅✅ 


#KaziNaUtuTunasongaMbele

#TunazimaZoteTunawashaKijani

#OktobaTunatiki✅✅✅

Post a Comment

0 Comments