EWURA Yawanoa Wasambazaji na Wauzaji wa LPG - Manyara

 


Na mwandishi wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) – Kanda ya Kaskazini, leo tarehe 21 Juni 2025, imeendesha semina kwa wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Mkoa wa Manyara.

Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Mha. Lorivii Long’idu, alieleza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wadau hao kuhusu umuhimu wa kuzingatia vigezo na masharti katika utoaji wa huduma za usambazaji na uuzaji wa LPG ili kuepuka madhara na kufungiwa leseni. 

Pia aliwataka wasambazaji wakuu (superdealers) nao kujenga tabia ya kuwapatia elimu wauzaji (dealers) kuhusu masuala ya usalama.

Mha. Long’idu alisema EWURA inaendelea kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ukilenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.

Mhandisi wa Petroli, Magreth Mwita, alitoa utaratibu wa kupata leseni ya kusambaza na kuuza LPG, na kuwasisitiza kuzingatia matakwa ya kisheria na ya kiufundi katika biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na mizani,  lakiri na kuepuka uchakachuaji.





Post a Comment

0 Comments