TUMETEKELEZA KWA KISHINDO ILANI YA CCM KATA YA MARUMBO - DIWANI MPENDU.

 




Na mwandishi wetu

Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM  kata ya Marumbo, wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani wamepitisha utekelezaji wa ilani ya 2020 -2025 uliofanyika katika ukumbi wa Kata. 

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji huo kwa kipindi cha Miaka mitano, diwani wa kata ya Marumbo Msafiri Mpendu amesema utekelezaji wa miaka mitano umefanyika katika sekta zote zinazoigusa jamii. 

Diwani Mpendu, ameelza  zaidi ya shilingi milioni 227 zimepelekwa katika sekta ya afya kwenye miradi ya ujenzi wa zahanati, nyumba za mtumishi, na usambazaji wa mifumo ya maji.

Katika sekta ya Elimu milioni 239 zimepokewa na kupelekwa katika maendeleo ya miundombinu ya elimu ikiwemo madarasa, vyoo na jiko la kisasa, pamoja na  ugawaji magodoro kwa wanafunzi kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe. 

Akizungumzia juu ya sekta ya Maji katika kata hiyo amesema wananchi wamenufaika na uchimbaji wa visima 16 vilivyochimbwa kimkakati ili kuhakikisha vinahudumia idadi kubwa.






Post a Comment

0 Comments