Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 8 Septemba 2025 amekutana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Asha Rose Migiro, Ikulu Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwinyi alimpongeza Dkt. Migiro kwa uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa na kueleza matumaini yake makubwa kutokana na uwezo wake wa kiuongozi. Aidha, alifurahishwa na mwenendo wa kampeni za CCM unaoashiria kukubalika kwa chama hicho na kuonesha taswira ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Vile vile, Rais Mwinyi alitumia fursa hiyo kumtakia mafanikio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni zinazoendelea kote nchini. Pia alishukuru CCM Makao Makuu kwa msaada mkubwa unaotolewa kuelekea uzinduzi wa kampeni za chama hicho Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika Septemba 13.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Asha Rose Migiro, ameahidi kushirikiana kwa karibu na CCM Zanzibar na kufanya kazi bega kwa bega kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa chama hicho katika uchagunzi mkuu.
0 Comments