Mkururugenzi mkuu wa Msd Ndugu Laurean R. Bwanakunu alisema kampuni ya deloitte imenukuliwa visivyo sahihi ripoti ya wataalam washauri kampuni deloitte iliyopewa jukumu na serikali oktaba 2015 ya kufanya mapito ya tathimini(strategic review) ya utendaji wa bohari ya dawa kwa minajili ya kuiboresha."Tunapenda kutoa taarifa kuwa sio kwamba dawa zenye thamani ya shillingi bilioni 11.7 zimekwisha muda wa matumizi, bali ni mkusanyiko wa dawa na vifaa tiba ambavyo vimekaa muda mrefu bila kuombwa na Vituo vya Afya kutokana na ama kutohitajika au kupitwa na teknolojia ya matumizi. Kundi hili la dawa na vifaa huitwa DOS (Dormant, Obsolete and Slow moving) ambalo linahusisha dawa kama vile vidonge vya Ketoconazole, Griseofulvin(zinazotibu magonjwa ya ngozi),na dawa za sindano za Procaine Penicillin Fortified(antibiotics). Pia vifaa na vifaa vya maabara kama Ferric Chloride, Volumetric pipettes, Acetic acid glacial na Film X- Ray"alisema mkurugenzi mkuu wa Bohari ya dawa Tanzania
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_fOgiLH06bQZI0JzD8fO4djuL1WJSvrMTSzlqEvK3E0BVGPULhnYDjqgw7DbqOLyRF_UgPc2inzwVLklQIO80Dwr2x8epuE9V4RWDXzZBOygDRb1vGOnSaVVAp0p2OvmBL8xnAJ-zMjQ/s320/MSD+warehouse+_RighttoHealthphoto_must+credit.jpg)
Eneo la Msd la kuhifadhi Dawa.
Gari mpya za Msd.
0 Comments