Wakazi Simiyu wapewa elimu ya uzazi wa mpango.............

 Wananchi wa kijiji cha itobo,itirima mkoani simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasiokuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi.Akizungumza katika mafunzo ya uzazi wa mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka maria stopes  Tanzania Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijijini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila ya mpangilio jambo linalofanya kuendelea kuwa maskini nukuu "Nawasa wanakijiji wa kijiji cha Mitobo Kuacha mila potofy za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleonunakuta mwanamke ana watoto 10-15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia"Alisema Meena
Pia Bi.Meena aliwashukuru wananchi wa kijiji cha mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango,akiongea baada ya kumaliza mafunzo Bi Meena alisema muitiko wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.
 Mtaalam wa musuala ya uzazi wa mpango kutoka Maria stopes Tanzania Bi. Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo,Itirma Mkoani simiyu mapema wiki iliyopita,Elimu hii ileenda sambamba na upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango.Picha  nimepigwa na Cathbert kujuna wa kajunason Blogspot
 mtaalam Bi. Meena akiwa anatoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo itirima Mkoani Simiyu.
 wananchi wa Itobo itirima MKoani Simiyu wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya Elimu ya uzazi wa mpango iliyotolewa na Maria stopes tanzania
 Wafanyakazi wa maria stopes Tanzania wakianda bango la tangazo ikiwa ni maandaliza katikaka eneo la utoaji elimu ya uzazi wa mpango kijiji cha itobo itirima Mkoani Simiyu.
wananchi wa kijiji cha itirima mkoani Simiyu wakiwa wanasikiliza kwa makini elimu ya uzazi wa mpango iliyotolewa na Maria stopes Tanzania.

Post a Comment

0 Comments