Jokate Awataka Vijana UVCCM Kupiga Kura kwa Weledi

 



Na mwandishi wetu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Jokate Mwegelo, ametoa Rai kwa wajumbe wa mkutano wa UVCCM kuhakikisha wanapiga kura kikamilifu na kuhakikisha wanachagua wawakilishi wa vijana kwa weledi.

‎Ameeleza hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa UVCCM Agosti 1, 2025, jijini Dodoma, wenye ajenda ya uchaguzi wa kura za maoni kwa ajili ya kuwachagua wabunge na wawakilishi kutoka kundi la vijana.

‎ “chaguzi wetu tunaufanya leo ni mchakato ambao unahusisha wajumbe kupiga kura, na kuchagua wale watakao tuwakilisha vijana zaidi ya milioni 35 katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Rai yangu kwenu tushiriki kupiga kura kikamilifu kwa kuwachagua wale watakao weza kuzibeba ajenda zetuna kuwajibika kwa maslahi yetu vijana wa CCM na vijana wa taifa lote kwa ujumla wake.” Jokate Mwegelo 

‎Aidha, Jokate amewataka vijana wa chama hicho kuendelea kuishi kwa ujamaa hata mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo.


#KaziNaUtuTunasongaMbele

#KijanaNaUongozi

#OktobaTunatiki✅✅

Post a Comment

0 Comments