JOKATE: TUCHAGUE WAGOMBEA WATAKAOBEBA AJENDA ZETU

 


Na mwandishi wetu


Katibu Mkuu wa UVCCM, Ndg. Jokate Urban Mwegelo amewasihi wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa UVCCM kuchagua wagombea wa Ubunge wa Viti Maalum kundi la Vijana ambao watabeba ajenda za vijana katika Bunge.

Ndg. Jokate amesema hayo leo tarehe 01 Agosti 2025 wakati akifungua mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Jiji, Dodoma.

“Uchaguzi wetu tutakaofanya leo ni mchakato ambao utahusisha wajumbe kupiga kura na kuchagua wale watakaotuwakilisha vijana zaidi ya milioni 35 katika Bunge, rai yangu tushiriki kupiga kura kikamilifu kwa kuwachagua wale watakaoweza kubeba ajenda zetu na kuwajibika,” amesema Jokate


#OktobaTunatiki

#KazinaUtuTunasongaMbele

#TunazimaZoteTunawashaKijani

Post a Comment

0 Comments