NA MWANDISHI WETU
Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu kupitiq Mkutano wake na Vyombo vya Habari katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma.
"COSTECH mwaka huu tumeleta wabunifu ambao tumekuwa tukiwafadhili kupitia mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU kwa miaka minne (4) ya nyuma tangu mwaka 2019, ambao bidhaa zao tayari zimeingia sokoni " alisema Dr Nungu.
Dkt. Nungu aliongeza kuwa ni muhimu kwa wadau wengine ambao hawakupata nafasi ya kufikiwa na COSTECH kutumia Jukwaa la Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa (Innovation Week) inayoendelea kuadhimishwa kuanzia tarehe 24 - 28 Aprili 2023 ili kutangaza bunifu zao kwa watanzania.
" Pia nitoe wito kwa wananchi, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuja kujionea na kuwekeza katika hizi bunifu, kuona kwenye kuendeleza ubunifu
" Vilevile tunayo Taasisi inayofanana na COSTECH toka Afrika kusini ambao tunakutana mara kwa mara kujifunza na kuna wakati tulishafadhili bunifu nyingine pamoja, nao pia wamekuja kushiriki ili kuipa hadhi Wiki ya Ubunifu kuongeza Sura ya Kimataifa " alisisitiza Dkt. Nungu
Alihitmisha kuwa Mwezi wa sita (6) COSTECH inategemea kuwa na Kongamano la Ubunifu maarufu kama STICE katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kituo cha Mwalimu Nyerere - JNICC, jijini Dar es Salaam.
0 Comments