Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Intermech Engineering Limited Mhandisi Peter Chisawillo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na mwandishi wetu
KAMPUNI ya Intermech Engineering Limited iliyopo mkaoni Morogoro imesanifu, kubuni na kuunda mashine ya kukausha muhogo.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 20, 2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mhandisi Peter Chisawillo akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya kuongeza thamani bunifu za hapa nchini iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) kwa ufadhili wa Taasisi ya FUNGUO.
Mhandisi Chisawillo amesema mashine hiyo imevumbuliwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Greenwich cha nchini Uingereza na kutengenezwa na Kampuni hiyo kwa ufadhili wa COSTECH.
“Kazi yetu ni kusanifu, kubuni na kuunda mashine za kusindika mazao ya kilimo, na sasa tumakuja na mashine ya kukausha muhogo, ya “Flush Dryer”,” amesema Mhandisi Chisawillo na kuongeza,
“Asili ya uundwaji wake ni kutoka Chuo Kikuu cha Greenwich cha nchini Uingereza na kutengenezwa na kiwanda chetu,”.
Amebainisha kwamba mashine hiyo inauwezo wa kukausha tani saba za muhogo kwa sikuambayo ni sawa na kilo 2100 za muhogo.
Mhandisi Chisawillo ameeleza kwamba wameamua kutengeneza mashine hiyo baada ya kuona changamoto ya kuharibika haraka kwa zao hilo muhimu, hivyo kuamua kuja na mashine hiyo ambayo itasaidia kukausha haraka na kuzuia kuharibika.
Kwa upande wake Mtaalam wa Mashirikiano kutoka COSTECH Promise Mwakale amesema lengo la Warsha hiyo ni kuongeza thamani ya bunifu za hapa nchini.
Amebainisha kwamba kwa ushirikiano na Vyuo kunaweza kukuza thamani hiyo ya bunifu kwamba hadi sasa ushabuniwa na kutengenezwa unga usio na sumu kuvu.
Kwamba kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kumesaida kubuniwa kwa Teknolojia ya Magamba ya kutengenezea ngozi nzuri na bora.
Hivyo Mwakale amesema kuwa ni dhahiri Vyuo vinaweza kusaidia kubuni teknolojia ambazo zinaweza kuongeza tahamani.
0 Comments