SERIKALI YAJIPANGA KUJA NA MPANGO MKAKATI KUKABILIANA NA MALARIA

 


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Rashid Mfaume akizungumza wakati akifunga semina ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyofanyika April 21, 2023 Jijini Dar es Salaam


Mratibu wa Udhibiti wa Maleria Mkoa wa Dar es Salaam Dokta Ford Chisongela akiwasilisha mada katika Semina ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyofanyika April 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Dar ea Salaam
Serikali imesema imejipanga kuja na mipango miradi  ya afua ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria nchini ikiwa ni pamoja na kuanza kutoa Dawa kinga kwa watoto wa shule za msingi ili kufikia malengo ya maambukizi kwa asilimia 0.

Akiwasilisha mada katika Semina ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyolenga kuwajengea uwezo kuelekea maadhimisho ya siku ya Maleria Duniani ambayo uadhimishwa kila mwaka tarehe April 25, kaimu meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti maleria kutoka wizara ya Afya Dkt. Abdallah Lusasi amesema hali ya maambukizi, vifo, pamoja na wagonjwa wanao lazwa imeshuka na mafanikio makubwa kuelekea mpango wa kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030.

Amesema serikali imekuwa ikichukua hatua na mikakati zaidi ya kupambana na Malaria zikiwemo upatikanaji wa Dawa na vyandarua, kupitia kitengo cha kampeni ya mapambano dhidi ya Malaria pamoja na kitengo cha utafutaji fedha na usimamizi wa miradi ya Malaria.

"Takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 94 wapo kwenye hali tofauti za maambukizi ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo ilikuwa ni asilimia 7.5 ya maambukizi, dhamira yetu ni kufika asilimia 3.5 mwaka 2025, Sasa tupo wapi tutasema mbele kwani kwa sasa ni Mikakati ni miwili tuliyojiwekea kwanza kuhakikisha tunapunguza wingi wa maambukizi na kutokomeza maleria ifikapo 2030,” Alisema Bw. Lusasi.

Kwa upande wake Mratibu wa Udhibiti wa Maleria Mkoa wa Dar es Salaam Dokta Ford Chisongela amesema mkoa wa huo licha ya kuwa ni miongoni mwa mikoa inayofanya vyema katika kudhibiti maleria bado kuna huitaji wa afua za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kugawa vyandarua kwa watu wasiojiweza ili kuhimiza matumizi ya vyandarua.

“Takwimu zinaonyesha Tuko asilimia 0.7 sawa na Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Iringa na Njombe, kwa hiyo tumepiga hatua kubwa sana lakini moja ya mambo ambayo yametuwezesha kufika huko ni matumizi ya vyandarua" Alisema Dkt. Chisongela

Alibainisha kuwa mkoa wa Dar es Salaam ulianza kunyunyizia viuwadudu kwenye mazalia ya mbu mwaka 1996. Mikoa mingine wameanza miaka mitatu iliyopita hii imesaidia kupunguza kiwango cha maleria pamoja na matibabu ambayo tunawapa wananchi wetu.

Kupitia mpango huo Ilala inaongoza kuwa na Maleria ikiwa na asilimia 1.7, ikifatiwa na Kinondoni na Ubungo ambazo Takwimu zao zinafanana, kisha Tameke na Kigamboni wao takwimu zinaonyesha wana maambukizi kidogo.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Rashid Mfaume akizngumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo amesema mkoa wa Dar es salaam upo tayari kwa ajili ya maadhimisho ya kitaifa ya malaria huku akiainisha baadhi ya mipango na hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha wanapunguza maambukizi hasa katika kata ya Msongora Ilala, na tungi Kigamboni, ambazo bado zina maambukizi ya juu licha ya kuwa miongoni mwa mikoa tisa iliyo chini kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Maadhimisho ya siku ya Maleria Duniani mwaka huu yatafanyika April 25 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yakiwa na Kaulimbiu isemayo ‘WAKATI WA KUTOKOMEZA MALERIA NI SASA, BADILIKA, WEKEZA, TEKELEZA’.


Post a Comment

0 Comments