WAZIRI CHANA MGENI RASMI USIKU WA TUZO ZA TMA APRILI 29, 2023, MAANDALIZI YAKAMILIKA

 


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dkt.Kedmon Mapana akizungumza na Wanahabari leo Aprili 27,2023 kutoa taarifa rasmi ya maandalizi ya Usiku wa Tuzo za muziki nchini (TMA) zinazotarajiwa kufanyika Aprili 29,20223  Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo  Dkt.Pindi Chana.


NA MWANDISHI WETU 


KATUBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana amesema Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Usiku wa Tuzo za muziki (TMA) Aprili 29,2023 Ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.

Dkt. Mapana amebainisha hayo leo Aprili 27,2023 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema mchakato wa tuzo hizo ulizunduliwa rasmi mapema mwezi Februari 2023 na ukawataka wasanii kupendekeza kazi zao ziingie kwenye Kinyang'anyiro hicho cha tuzo kwa mwaka 2023.

"Wasanii wengi waliojitokeza kupendekeza kazi zao ambapo kwa mwaka 2023 zaidi ya Kazi 1700 ziliweza kukusanywa ."

Hata hivyo Mapana amesema Usiku huo ni mahususi kwa watu mahiri zaidi pia akaongeza kuwa jumla ya tuzo 52 zitatolewa siku hiyo.

"Tutakuwa na vyeti vya taasisi ambazo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika muziki pia Usiku huo watatambuliwa pamoja na wasanii ambao wataibuka washindi kwenye vipengele vya tuzo watapatiwa tuzo zao."

Aidha Mapana amewaambia wasanii na wadau wa Sanaa kujitokeza kwa wingi mapema Aprili 28,2023 katika ukumbi wa "Superdome" kwa ajili ya Semina kuelekea Kilele cha Usiku wa tuzo hizo.


Post a Comment

0 Comments