RAIS WA KOREA KUSINI AMEOMBA RADHI KWA MSURURU WA SAKATA ZINAZOMKABILI MKE WAKE

 


Na mwandishi wetu

Rais wa Korea Kusini ameomba radhi kwa msururu wa sakata zinazomkabili mke wake ambazo ni pamoja na kudaiwa kukubali mkoba wa kifahari wa Dior na uingiliaji wa kubadilisha thamani ya hisa .

Akihutubia taifa kwenye runinga, Yoon Suk Yeol alisema mke wake, Kim Keon Hee, alipaswa kuonesha uadilifu zaidi, lakini akasema baadhi ya madai dhidi yake "yalitiwa chumvi".

Rais alisema ataunda ofisi ya kusimamia majukumu rasmi ya mke wa rais, lakini akakataa wito wa uchunguzi kuhusu shughuli zake.

Hatua ya Yoonkuomba radhi inajiri wakati anajaribu kuimarisha umaarufu wake miongoni mwa wananchi wa Korea Kusini ambao umedorora kwa kuhusishwa na sakata zinazomkabili mke wake.

Mwishoni mwa 2023,Chaneli ya mrengo wa kushoto ya YouTube ya Voice of Seoul ilichapisha video ambayo ilidaiwa ilionyesha Kim akikubali mkoba wa Dior wa thamani ya milioni 3 ($2,200; £1,800) kutoka kwa mchungaji, ambaye alirekodi mazungumzo hayo mnamo Septemba 2022 kwa kutumia kamera iliyofichwa kwenye saa yake.

Mnamo Februari, Yoon alisema kwamba kanda hiyo ilivuja kama "hila ya kisiasa", na hakuomba msamaha.

Post a Comment

0 Comments