ULEGA AWASILI ARUSHA, APOKELEWA NA RC MAKONDA.

 




Na mwandishi wetu

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ameanza ziara ya kikazi mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda.

Akiwa Katika Mkoa huo Waziri Ulega atatembelea na  kukagua barabara ya Mianzini-Ngaramtoni (KM18), inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri Ulega ameambatana na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour na Viongozi waandamizi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS).




Post a Comment

0 Comments