Na mwandishi wetu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa Ilani ya Uchaguzi ilieleza Kufanyika Ukarabati wa Uwanja wa Amani pekee lakini Serikali imevuka Malengo kwa Viwanja vya Wilaya na Inalenga kujenga Academy kila Mkoa.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ukarabati Mkubwa wa Uwanja wa Gombani na Viwanja vyengine Wilaya ya Chake chake , Mkoa wa Kusini Pemba.
Aidha , Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa hatua ya Kuvikarabati Viwanja vya New Amaan Complex, Mao Tse Tung na Gombani na Ujenzi wa Viwanja 17 kila Wilaya Unalenga kuibua Vipaji Nchi Nzima Katika Ngazi Zote
Rais Dk. Mwinyi amesema umefika Wakati kwa Zanzibar Kuzalisha Vipaji vya Vijana watakaokuwa na uwezo wa kucheza Nje ya Nchi.
Halikadhalika, Rais Dk.Mwinyi amefafanua kuwa Wachezaji Wakubwa wanaotamba katika ligi za Uingereza , Hispania na Italia wametoka katika Academy za Soka katika nchi zao jambo alilolielezea kuwa ni lazima lifanyike Zanzibar.
Amepongeza kuwa Serikali inaweka Mkazo katika Ukarabati wa Uwanja wa New Amani Complex utumike ipasavyo katika Michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Mwezi wa Februari na Michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika Mwaka 2027 Tanzania Ikiwa Mwenyeji kwa kushirikiana na Uganda na Kenya.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameitakia kila heri Timu ya Taifa ya Zanzibar ZANZIBAR HEROES inayoshiriki Michuano ya Mapinduzi kufanya vema na Kushinda Kombe hilo.
Uwanja wa Gombani Unafanyiwa Ukarabati Mkubwa ikiwemo Uwekaji wa paa jipya ,Ujenzi wa kuta ,Vyumba vya Wachezaji,Eneo la Watu Mashuhuri, Maegesho,Tartan ,Uwekaji wa Minara, Mifumo ya Maji na Umeme pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa Mazoezi pembezoni mwa Uwanja huo.
Ukarabati huo wa Awamu ya Pili utagharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 4,250,000 unafanywa na Kampuni ya REFORM SPORTS ya Uturuki.
0 Comments