WANACHAMA 602 WA CHADEMA WAJIONDOA UANACHAMA

 



Na mwandishi wetu 

Jumla ya wanachama 602 waliojiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni wakitokea Chama cha Wananchi (CUF) Kata za Mwananyamala na Buguruni Jijini Dar es Salaam hii leo Mei 6, 2023 wametangaza kujiondoa uanachama wa CHADEMA huku wakitaja sababu kubwa kuwa ni ukiukwaji wa  makubaliano na kutopewa ushirikiano na baadhi ya viongozi wa ngazi za chini wa CHADEMA.


Ambapo Kata ya Mwanayamala ni Wanachama 402 na Kata ya Buguruni ni 200

Wanachama wakiongea mbele ya vyombo vya Habari walisema kuwa sababu kubwa za kujiondoa uanachama ni ukiukwaji wa makubaliano  na kutopewa ushirikiano na baadhi wa viongozi wa ngazi za chini wa Chadema, Huu ni mwendelezo wa wanachama kujiondoa katika chama hicho  ikitajwa sababu ni kutokuwepo na uongozi mzuri wa uendeshaji wa chama hicho. 



PICHA MBALIMBALI







Post a Comment

0 Comments