CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI MTOTO WA KITANZANIA/SAVE THE CHILD YAZINDUA KAMATI YA USHAURI KWA MTOTO

 



Na Mwanahabari wetu,Mikocheni Dar.

IMEELEZWA kuwa bado watoto wa kitanzania wananyimwa fursa ya kuyasemea matatizo yao yanayowazunguka jambo linalochangia kushinda kutatuliwa changamoto zao.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu shirika lisilo la kiserikali la  the save children Tanzania,Angela Kauleni,wakati wa uzinduzi wa kamati ya ushauri ndani ya shirika hilo lengo likiwa ni kusikiliza maoni na ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa watoto na hivyo kuchagiza ustawi wao na wa jamii kwa ujumla. 

Aidha,Kauleni,amesema watoto wakitanzania walikuwa wanakosa sehemu ya kusemea matatizo yao hivyo ujio wa kamati hiyo itasaidia watoto kueleza na kushauri nini kifanyike kuhusu maisha yao kiujumla.

"Watoto wamekuwa wakinyimwa fursa kusema changamoto zao,lakini ujio wa kamati hii itatusaidia kutambua changamoto zao,na tunaamini tunajukwaa maalum la watoto"Amesema Kauleni.




Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Children,Ian Vale,amesema wamejidhatiti katika kuongeza ushiriki wa watoto kwenye kutoa maamuzi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayowahusu hali itakayowezesha kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakumba


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo,Tatu Ramadhani,ameishukuru Save the chirdren kuja na kamati hiyo na kusema kamati hiyo itasaidia wao kutatua changamoto zao zinazowakumba.




Post a Comment

0 Comments