DKT,SAMIA APEWA KONGOLE KWA KUENDELEA KUTOA FURSA

 


Na Richard Mrusha 


KATIBU  mkuu wa shirikisho la vyama vya wachimba madini Tanzania Amesema wanamshukuru rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa mwendelezo wa mikutano hiyo ambayo Kwa muda Sasa imekuwa ikifanyika na imekuwa ikileta mabadiliko makubwa Sana .


Amesema kuwa imefika mahala Sasa Rais DKT. Samia amekuwa akitoa fursa Kwa watanzania kuweza kupata mashirikiano kutoka Kwa wadau wa madini wa ndani ya nchi na  nje ya nchi


 Katibu huyo washirikisho ameyasema hayo oktoba 25 jijini Dar es Salaam katika kongamano la madini la kimataifa ambalo linafanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere .


Amesema mkutano huo umekuwa wakimataifa kabisa ,wengine kutoka ulaya na wengine kutoka mataifa mengine ya kiafrika wameweza kushiriki na nchi za mbali kabisa nakwamba hiyo inaleta nafasi ya kipekee hasa wachimbaji wadogo kuweza kupata msaada wa kimitaji  kama fedha na uwekezaji lakini pia kupata teknolojia mbalimbali.


Pia Amesema teknolojia hizo Sasa zinaweza kuwafuata nyumbani badala ya kwenda kuitafuta mbali lakini kubwa zaidi kuweza kupata masoko ya madini na kwasababu kongamano hilo limeweza kupata hata wanunuzi mbalinbali wa kimataifa wamadini hivyo ni nafasi ya kipekee na ninafasi ya wao kuweza kuelezea kutoka Kwa wadau wenyewe hali halisi ya kichimbaji nchini .umiliki wa leseni madini ambayo yapo Ili waweze kutembelea .


"Kuhusu fursa zinazojitokeza kwanza anamshukuru sana Rais Dkt Samia na kimsingi Dunia inaona,nchini yetu inaona kimsingi nchi yetu imetulia Kwa uongozi wa mama ameamua kuwafungulia watanzania waende Duniani waweze kushiriki uchumi wa Dunia na hii imeleta maana kwamba Hawa wengine waje Moja Kwa Moja ili kuwaletea watanzania waone na ndio maana mikutano hii mikubwa imekuwa ikija na inatufungulia "Amesema 

.

Nakuongeza kuwa mikutano hii maana yake ni Moja tu inaenda kupiga msitari Kwa lengo la kuleta nchi nyingine Kwa ajili ya kupiga maendeleo ya watu wake ili kufanya Dunia iendeleee kuwa salama kiuchimu."amesisitiza katibu.





Kwa upande wake Mwenyekiti wa Dacorema Josephati mkombachepa Amesema kuwa mikutano hiyo imesaidia sana na kwanza inewafanya wakutane na watu wakutoka  nchi mbalimbali hasa katika ukanda wa SADEC wamekutana hapo .


Amesema katika ufunguzi wa mkutano huo Sasa unakwenda kutoa fursa na huko nyuma Kwa upande wa Afrika mashariki walikuwa hawana mikutano mikubwa Kama hiyo lakini kwasasa imekuwa ni ufunguo hasa hapa nchini na kwasasa zinapatikana nchi zingine   za nje ya Tanzanaia Kwa lengo la kujadili maendeleo ya nchi zingine nje ya Tanzania .


Mkombachepa Amesema wao kama femata wamefanya uimarishaji wa mambo hayo Kwa muda mrefu na Sasa hivi kupitia mkutano huo wakitoka wanakwenda kufanya mambo makubwa na wanakwenda kukaa Ili kujadili cha kufanya na hasa kwenda kujadiliana kuhusu tamko la Serikali la ajenda ya 20230 kwenye sekta ya madini  


Post a Comment

0 Comments