WIKI YA AZAKI 2023 KUWAKUTANISHA WADAU ZAIDI YA 500 JIJINI ARUSHA

 


Na mwanahabari wetu


ZAIDI ya washiriki 500 kutoka kwa wadau wakuu wa Maendeleo katika Sekta ya Asasi za kiraia/AZAKI, Sekta Binafsi, Serikali na wananchi wanatarajia kushiriki wiki ya AZAKI 2023 itakayofanyika Oktoba 23-27 jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 17, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Wiki ya AZAKI 2023 itakuwa na fursa nyingi za kujumuika pamoja kama Sekta ya AZAKI na wadau wake wote na ni fursa ya kipekee ya kufikiria, kuchangamana na wadau wa Maendeleo,” amesema Kiwanga na kuongeza,

“Wiki ya AZAKI inaleta pamoja Asasi za kiraia, Serikali, wananchi, wanazuoni na Sekta Binafsi kujadili masuala ya yanayohusu Maendeleo ya Taifa,”.

Kiwanga amebainisha kwamba kauli mbiu ya Wiki ya AZAKI 2023 ni teknolojia na jamii. Kwamba katika wiki ya AZAKI wataangalia walipotoka, walipo sasa na wanakwenda wapi.

Kwamba kauli mbiu hiyo inasisitiza lengo la kuzileta pamoja asasi za kiraia, watunga sera, wanateknolojia na wadau kubadilishana mawazo, uzoefu na maarifa juu ya matumizi ya teknolojia kwa matokeo chanya ya kijamii nchini.

Amesema sababu za kuchagua kufanyika wiki hii mkoani Arusha ni kwasababu walifanya wiki ya AZAKI 2022 jijini Arusha, kuwepo kwa Taasisi za Kimataifa, ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mahakama ya Afrika na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki na ukaribu wa Arusha na nchi nyingine za Afrika Mashariki na umakini.

Ameeleza kuwa washiriki wengi zaidi watatoka katika AZAKI na wengine ni wawakilishi kutoka Wizara, Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali, watunga sera, vyombo vya habari, wanataaluma na Sekta Binafsi.

Pa amesema zitafanyika kuhusu ya kuwaalika washiriki wengine kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwamba katika wiki ya AZAKI watakuwa na mada tofauti zilizojikita katika kutathimini kauli mbiu ya teknolojia na AZAKI.

Ametaja maeneo ya mada za Kongamano kuwa ni ujumuishaji na uwezeshaji wa kidigitali, Matumizi ya takwimu kuleta manufaa kwa jamii, teknolojia na utetezi wa kijamii, elimu na mafunzo ya kidigitali nchini Tanzania na teknolojia katika ushirikiano na kuboresha uwazi.

Nyingine ni ujasiriamali na teknolojia kwa Maendeleo endelevu, kuimarisha Usalama wa mtandaoni, kuwekezesha wanawake na Vijana kupitia teknolojia, kuweka wazi data na uwazi kwenye utawala na kutumia maarifa bandia (AI) yanayozingatia maadili kwa manufaa ya jamii.

Kwa upande wake, Doreen Domic kutoka Stanibic Banki amesema kuwa, wao kama taasisi binafsi ya kifedha wamefurahi kuwa sehemu hiyo ya azaki katika kushiriki.

Naye, Nuria Mshare,  Mwakilishi mkazi ambae ni mshauri wa azaki amesema wiki hiyo itawaleta wadau mbalimbali kujadili masuala ya teknolojia inavyosaidia vijana kugeuza kuwa fursa kiuchumi.







Post a Comment

0 Comments