HIZI HAPA KAMPUNI TATU ZA KITALII "TWENZETU KILELENI 2023".

 



Na. Andrew Chale.

KATIKA kuelekea kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania, maandalizi ya kujiweka katika historia kwa kupanda Mlima Kilimanjaro “Paa la Afrika” ambapo tayari baadhi ya kampuni za Utalii wameonesha uzalendo wao wa kukamilisha hilo.

Kwa mujibu wa waratibu wa shughuli hizo kutoka Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),Afisa Mhifadhi Mkuu Gladys Ng'umbi, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro azimezitaja kampuni za Zara Tours, African Scenic na African Zoom ambazo kila moja itakuwa na njia yake.

"Tofauti na miaka mingine iliyopita mwaka huu tutatumia njia tatu tofauti kuelekea kilele cha mlima Kilimanjaro. Kampuni hizi zinakufikisha katika kilele kwa gharama ya kitanzania kabisa.

"Kampuni ya ZARA Tours watakupeleka mpaka kileleni kupitia njia ya Marangu kwa gharama ya kitanzania ya Shillingi 1,150,000/= (kwa siku 6).


Lakini pia Kampuni ya Afrikan Zoom watakupeleka mpaka kileleni kupitia njia ya Machame kwa gharama ya kitanzania ya shillingi 1,570,000/=(kwa siku 7)

Na mwisho ni kampuni ya Afrikan Scenic watakupeleka mpaka kileleni kupitia njia ya Lemosho kwa gharama ya kitanzania ya shillingi 1,700,000/=(kwa siku 8)." Amesema Afisa Mhifadhi Mkuu Gladys Ng'umbi, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro

Na kuongeza: "Jiunge nasi, tukwee kilele cha mlima Kilimanjaro na tutangaze kwa sauti moja: Miaka 62 ya Uhuru, mnaweza wasiliana kupitia +255(0)739767679 ili kuweza kuwa miongoni mwa watakaopanda" Amesema Afisa Mhifadhi Mkuu Gladys Ng'umbi, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.

Zoezi hilo linasubiriwa kwa shauku kubwa ya kuhakikisha kila mmoja anakwea kilele cha mlima huo.




Post a Comment

0 Comments