WAOGELEAJI 30 KUSHIRIKI MASHINDANO YA 8 YA AFRICA AQUATICS KANDA YA III KIGALI, RWANDA

 


Na Isiaka Hamis Kikuwi


KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameikabidhi bendara Timu ya Taifa ya kuogelea kwa ajili ya kuiwakisha Tanzania kwenye mashindano ya nane ya Afrika Aquatics kanda ya tatu (3) yatakayofanyika nchini Rwanda.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi bendera hiyo iliyofanyika Novemba 20, 2023 katika Bwawa la Kuogelea la IST jijini Dar es Salaam Msitha ameitaka timu hiyo ikaliwakilishe vyema Taifa na hatimaye warejee wakiwa washindi.

“Kwa Jinsia mlivyojiandaa naamini mtatuwakilisha vyema na mtarejea mkiwa mabingwa,” amesema Katibu Mtendaji wa BMT Msitha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Kuogelea Tanzania (TSA) Mhandisi David Mwasyoge amesema timu hiyo itakuwa na msafara wa waogeleaji thelathini (30), makocha watatu (3), na viongozi sita (6) watakaosafiri na kwamba mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia Novemba 23 mpaka 25 mwaka huu.

“Tanzania itatetea ubingwa wake dhidi ya timu 11 kwenye mashindano hayo baada ya kuibuka washindi Novemba mwaka jana,” amesema Mhandisi Mwasyoge.

Akibainisha msafara mzima wa timu hiyo amewataja waogeleaji kuwa ni Santo Bash, Aryan Bhatbhat, Lorita Borega, Amylia Chali, Filbertha Demello, Mahek Desai, Crissa Dilip, Romeo-Mihaly Mwaipasi, Sahal Harunani, Bridget Heep, Peter Itatiro, Michael Joseph, Aliyana Kachra na Aminaz Kachra.

Wengine ni Kaysan Kachra, Natalia Ladha, Audrey Makwaia, Myra Makwaia, Julis Missokia, Max Misokia, Zainab Moosajee, Luke Okore, Austin Okore, Enrico Barreto, Delbert Ipilinga, Aaliya Takim, Juanita Viljoen, Nicolene-Melony Viljoen, Collins Saliboko na Muskan Gaikwad.

Amewataja makocha kuwa no Alexander Mwaipasi ambaye ni Kocha mkuu, Michael Livingstone na Zubery Yusuph huku mameneja wakiwa ni Nadejda Kachra ambaye ni Meneja wa Timu, Carmen Demello – Meneja wa wachezaji, Maiju Missokia – Matron na Abraham Okore  - Patron.

Viongozi  amesema ni, Eng. David Mwasyoge – Rais TSA, Jeremiah Keema–m/kiti kamati ya maendeleo na elimu TSA na Amina Mfaume – Mkurugenzi wa Ufundi TSA.

Amesema malengo ya Tanzania kwenye mashindano ya kanda ya tatu ya Afrika Aquatics huko Kigali, Rwanda ni kuongeza maendeleo ya mchezo wa kuogele nchini.

Kwamba kwa kushiriki kwenye mashindano haya Tanzania itafaidika kwa kuongeza ubora wa michezo, vile vile Tanzania inataka kuonesha vipaji vya waogeleaji wake kwenye ngazi ya ukanda katika kuongeza kujituma ili kufikia ubora wa juu kwenye mchezo wa kuogelea.

Kadhalika amesema kushiriki kwenye mashindano kama haya ya Africa Aquatics kanda ya 3 kunawapa waogeleaji wa kitanzania ufahamu mkubwa zaidi juu ya mashindano makubwa na kuwaongezea uzoefu wa kushindana kimataifa.  

Kwamba Uwezo wataonesha waogeleaji wa Tanzania Kigali, Rwanda unategemewa kuongeza fahari na sifa ya Taifa kweye mchezo wa kuogelea na kuwapa motisha vijana na taifa zima kwa ujumla kushiriki kwenye michezo ya kwenye maji.

Naye Kocha wa Timu hiyo ya Taifa Alexander Mwapasi ameesema timu yake imejiandaa vizuri na anaamini itafanya vizuri.






Post a Comment

0 Comments