Na Mwandishi Wetu
Tanzania inashiriki katika mkutano wa 47 wa Shirika la Miliki Ubunifu Afrika (ARIPO) unaojadili taarifa ya mwaka pamoja na kupitisha mpango kazi wa mwaka 2024.
Washiriki wa mkutano huo wa siku nne unaofanyika Gaborone Botswana ni Wakuu wa Ofisi za Miliki Ubunifu kutoka nchi wanachama wa ARIPO, ambapo kwa upande wa Tanzania Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa ameongoza Msafara wa Tanzania kwa kuambatana na Maafisa wa BRELA Bw. Seka Kasera na Bw. Alex Mashamba huku upande wa Zanzibar ukiwakilishwa na Bw. Mustafa Haji kutoka Wakala Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA).
Mkutano huo wa siku nne unaohudhuriwa na nchi wanachama 22 za Afrika umefunguliwa rasmi leo tarehe 20 Novemba, 2023 na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Botswana Mhe. Mmusi Kgafela na utafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa ARIPO.
Katika mkutano huo ARIPO itawasilisha taarifa ya utendaji kazi ya mwaka kwa wanachama ambayo itajadiliwa na Wanachama na kuipitisha kisha kuwasilisha mpango kazi kwa mwaka 2024.
0 Comments