KAMATI YA BUNGE YAFANYA UKAGUZI KIWANDA CHA MAJI YA UHURU PEAK/SUMA JKT YAWAJIBIKA MAWAZO YA KAMATI HIYO

 




Na Isiaka Hamis Kikuwi 


Kamati ya kudumu ya Bunge ya mambo nje, Ulinzi na usalama imefanya ukaguzi katika kiwanda cha uzalishaji wa maji ya Uhuru Peak kilichopo chini ya SUMA JKT,Tukio hilo limefanyika leo Jumanne November 14,2023 katika kiwanda hiko kilichopo Jkt Mgulani, Temeke Jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kuwasilisha mawazo ya kuongezeka kwa uzalishaji wa maji na uboreshaji wa kifungashio cha chupa ya maji hayo.Kamati hiyo imewasili kiwandani hapo na kupokelewa na mwenyeji wake Jeshi la kujenga Taifa (JKT) kisha kuelekea Moja kwa Moja kiwandani(Plant)kujionea mawazo yao yametekelezwa.





Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kamaliza ukaguzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Victor Kawawa amesema"Tumekuja kukagua kiwanda hiki baada ya kupokea taarifa kwamba yameshakamilishwa yale mawazo ambayo yametolewa huko nyuma na Kamati kwamba waongeze uzalishaji wa maji"




"Ni huko awali walikuwa wanazalisha maji Lita 3250 kwa saa lakini sasa hivi baada ya kufunga mitambo mipya yenye uwezo mkubwa wanazalisha Lita 10,000 kwa saa na wamebadilisha muonekano wa chupa mbalimbali na aina za ujazo wa chupa mbalimbali kulingana na soko linavyotaka"alisema Victor Kawawa


Aidha Mwenyekiti Victor Kawawa ametoa Rai kwa mashirika,wizara na taasisi za kiserikali wanunue maji ya uhuru na wawaunge mkono ili kuendeleza azma ya shirika hili kuendelea katika soko na pia Kamati ya Bunge imewapongeza Jkt Suma na kuwahakikishia kuwa Kamati imeridhika baada ya kuona kuwa wamewekeza billion Moja na million mia sita kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda hiko.





Kwa upande wake,Mkuu wa SUMA JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMA JKT,Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele amesema"Mawazo haya ya upanuzi wa kiwanda hiki yalikuwepo ila Kamati imeweza kushinikiza utekelezaji wa upanuzi na kuhakikisha tunapanua hiki kiwanda ,Kwa hiyo baada ya kuwa tumekipanua Kamati alisema inataka kuja kuona kile ambacho walishauri na kama kweli tumetekeleza kama walivyokuwa wameagiza,Leo wamethibitisha na kuridhishwa na utekelezaji huo"

"Mpango wetu ni kuhakikisha maji ya uhuru yanawafikia mikoa yote Tanzania,Kwa sasa hivi mikoa yote ambayo inapitiwa na reli ya kati tayari tumeshaweka mkataba na TRC watakuwa wanatusafirishia maji yetu kwa gharama ile ile kwamba bei ya kushushia haya Morogoro haina tofauti na kushushia maji haya kigoma kwetu sisi ni advantage na tayari tameshafanya majaribio TRC wametusafirishia maji mpaka Dodoma na biashara imeenda vizuri"amesema Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele 


Kwa Tukio hili Jkt Suma wameweka historia mpya kwa kupanua kiwanda na kuongeza uzalishaji na zaidi kubadilisha muonekano wa chupa na aina mbalimbali za ujazo kuanzia milimita 350  mpaka Lita 50.

Picha mbalimbali za Tukio la ziara hiyo.










Post a Comment

0 Comments