MAWAZIRI WA FEDHA NA JINSIA KUTOKA AFRIKA KUKUTANA NCHINI,KUJADILI UFADHILI WA USAWA WA KIJINSIA.

 


Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza na wanahabari kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF Afritac East), utakaofanyika jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 15 hadi 17, Novemba, 2023


Na Isiaka Hamis Kikuwi 

Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 Afrika wanataraji kukutana nchini Tanzania katika mkutano wa kujadili namna bora ya kushughulikia athari za mapungufu ya kijinsia katika uchumi.

Nchi zinazotarajiwa kushiriki Mkutano huo utakaoanza Nov,15-17 mwaka huu jijini Dar es salaam ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda. 

Wakizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Doroth Gwajima, wamesema kuwa mkutano huo unalenga kujadili kuhusu namna yakuwawezesha wanawake na wasichana kiuchumi na kijamii kupitia ufadhili wa usawa wa kijinsia.

Waziri wa Fedha Dkt Nchemba amesema mkutano wa Mawaziri utaangazia hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na Jukwaa la Usawa wa Kijinsia, athari za uchumi jumla katika usawa wa kijinsia na jukumu la upangaji bajeti unaozingatia jinsia.

‘matokeo yanayotegemewa kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa Mawaziri ni uwepo wa vipaumbele vya kuharakisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na ahadi ya kugharamia utekelezaji kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo’amesema Dkt Nchemba



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Doroth Gwajima akizungumza na wanahabari kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF Afritac East), utakaofanyika jijini Dar es Salaamkuanzia tarehe 15 hadi 17, Novemba, 2023



Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Doroth Gwajima matokeo yanayotegemewa kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa Mawaziri ni uwepo wa vipaumbele vya kuharakisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na ahadi ya kugharamia utekelezaji kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo.





Mkurugenzi wa IMF - Afritac East, Bi. Xiangming LI, akizungumza wakati wa Mkutano na wanahabari kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Afrika wanaohusika na Masuala ya Fedha na Jinsia kutoka nchi 22 wanachama wa Jukwaa la Usawa wa Kijinsia (UN Women) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF Afritac East), utakaofanyika jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 15 hadi 17, Novemba, 2023

Mkurugenzi wa IMF Afritac East,Xiangming LI amesema mchango wa wanawake katika uchumi umekuwa mdogo ikilinganishwa na wanaume Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya Usawa wa Kijinsia (UN-Women),Hodan Addou akisema Shirika hilo litaongeza ufadhili katika masuala ya usawa wa kijinsia ili kuwawezesha wanawake na wasichana kutoka nchi wanachama

Hata hivyo imeelezwa kuwa  matokeo yanayotegemewa kwenye mkutano huo wa ngazi ya juu wa Mawaziri pia ni uwepo wa vipaumbele vya kuharakisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na ahadi ya kugharamia utekelezaji kutoka kwa washiriki wa Mkutano huo.







Post a Comment

0 Comments