MWONGOZO WA CHAKULA NA ULAJI WAZINDULIWA RASMI NCHINI TANZANIA.

 


Na Isiaka Hamis Kikuwi

Dar es salaam.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amezindua mwongozo wa Kitaifa wa Chakula na ulaji ulioandaliwa ili boresha matumizi sahihi ya Chakula mchanganyiko katika kutokomeza changamoto zote za utapiamlo na udumavu nchini.

Ambapo amesisitiza jamii kuondokana na dhana kuwa lishe bora ni gharama kubwa kwani vyakula vyote vinavyojumuishwa kupata mlo sahihi vinapatikana kwenye jamii yote nchi,kikubwa ni kufahamu mlo sahihi na kamili ni upi.

Akizungumza leo Novemba 16, 2023 katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika soko la kisutu Jijini Dar es Salaam Waziri Ummy amesema mwongozo huo umeandaliwa kwa kutumia taarifa na Takwimu za kisayansi zilizofanyika nchini na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 barani Afrika ambazo zinamuongozo kama huo.



Nimefahamishwa kwamba mwongozo huu uliandaliwa kwa kuhusishwa Wadau mbalimbali kutoka ngazi zote. Pia wananchi wa kawaida walipata fursa ya kutoa maoni yao kwenye jumbe na michoro mbalimbali iliyotumika kwenye mwongozo huu,” amesema Waziri Ummy na kuongeza

"Leo kwa kipekee kabisa ninawashukuru FAO na Umoja wa Ulaya kwa mchango wao mkubwa katika kuunga mkono juhudi zetu za kuboresha hali ya lishe kwa Watanzania na kwa kufadhili maandalizi ya mwongozo huu. Asanteni sana FAO na Umoja wa Ulaya,” ameshukuru Waziri Ummy.



Ametoa wito kwa viongozi hususan katika ngazi za Mikoa na Halmashauri kuhakikisha kuwa mwongozo huo unasambazwa na kutumika kikamilifu kwa kuwafikia wananchi wote.

Kadhalika ameielekeza Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) washirikiane na kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kuandaa jumbe fupi fupi zinazoweza kutumika katika vyombo mbalimbali vya habari kama vile Televisheni, Redio, Magazeti na Mitandao ya kijamii ili kufikisha ujumbe mahususi wa mwongozo huo.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe TFNCD Dkt.Germana Henry Leyna amesema mwongozo huo umeandaliwa ukiwa na taarifa za kina zitazomwezesha mlaji kupata taarifa sahihi zitazomwezesha mlaji kupata lishe bora.

Ameongeza kuwa mwongozo wa chakula na ulaji unaonyesha makundi yote ya vyakula ambavyo vinavyopatikana katika jamii hivyo hakuna mtu atakae hangaika kuvipata kwa shida.

Post a Comment

0 Comments