NAIBU KATIBU MKUU OMAR AZINDUA MNADA WA KWANZA MTANDAONI WA CHAI WA TANZANIA

 


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed Omar akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mnada wa Chai wa Tanzania jijini Dar es Salaam.


Na Isiaka Hamis Kikuwi

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed Omar amezindua rasmi mnada wa Chai wa Tanzania jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo leo Novemba 13, 2023 Dkt. Omar amesema kuwa uzinduzi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwekeza fedha nyingi kwenye Maendeleo ya Kilimo nchini.

Dkt. Omar ameipongeza Bodi ya Chai Tanzania kwa hatua hiyo kwani ni hatua kubwa kwa ukuaji wa Kilimo cha zao la chai nchini na kwamba Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatambua kazi kubwa iliyofanywa na Bodi hiyo pamoja na wadau wengine ikiwemo Sekta binafsi.

“Nitoe rai kwa wakulima na wazalishaji wa chai nchini kuazalisha chai bora ili kuweza kunufaika na mnada huu kwa Kufikia Masoko ya ndani na nje,” amesema Dkt. Omar na kuongeza,

“Serikali inatambua mnada huu utakuwa na manufaa makubwa kwa kuongeza thani ya zao la chai nchini,”.

Naibu Katibu Mkuu huyo amebainisha kwamba kuanza kwa mnada huo na hatua kubwa kwa ustawi wa zao hilo na kukuza uchumi wa mkulima/mzalishaji wa chai na Nchi kwa ujumla.

Kadhalika amesema moja ya lengo la mnada huo ni kuongeza mauzo ya chai ya nje Kufikia dola nilioni tano.

Ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuweka Mazingira wezeshi kwa ajili ya kuwezesha uwekezaji kwenye Kilimo cha chai Nchini.

Dkt. Omar amebainisha kuwa ili mnada huo uwe endelevu ametaka Taasisi zinazosimamia zao la chai zisimamie ubora wa zao hilo, lakini pia usimamizi wa uuzaji wa chai kupitia mnada angalau ufikie asilimia 15.

Kadhalika ametaka Nchi nyingine hususan Nchi jirani zishawishiwe kutumia mnada huu wa Tanzania kuuza chai yao pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani wa zao hilo ili kuchochea wazalishaji wa chai kuongezeka.

Amewataka Wenye Viwanda vya chai kuhakikisha wanawalipa Fedha zao wakulima na wazalishaji wa zao hilo, wenye mashamba ya chai waongeze uzalishaji, pamoja na Wenye Viwanda kuhakikisha wanaimarisha mitambo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania Mary Kipeja amesema kwamba pamoja na kuchelewa kuanza kwa mnada huo lakini anaamini itakwenda vizuri kwani wameanza vizuri.

“Mnada huu utakuwa na manufaa mengi sana, hii itawashawishi hata wasindikaji wa chai kuja nchini kwa wingi kwani gharama zitapungua na faida ya zao la chai itaongezeka. Hata mkulima mdogo atapata faida,” amesema Kipeja.

Kipeja ametaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mnada huo kuwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti wa kuutangaza hadi nje ya Nchi, ufinyu wa bajeti ya kusajili na kuwapatia wakulima vyeti vya ubora ili Kufikia viwango vya kimataifa.

Nyingine ni ufinyu wa bajeti ya kutumika katika kushawishia Nchi za jirani kutumia mnada wa Tanzania kuuza chai yao.





Post a Comment

0 Comments