NBS: WATAKWIMU WAPATIENI VIONGOZI TAKWIMU SAHIHI KUEPUKA UPOTOSHAJI

 




Na mwandishi wetu,Dodoma

WATAKWIMU wa Halmashauri, Wizara, Idara naTaasisi za Umma wametakiwa  kufanya kazi ya ziada kwa kuwapatia viongozi wao takwimu sahihi ambazo zimepata kibali kutoka Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS),lengo likiwa ni ili kuepuka upotoshaji wa takwimu wanapowasilisha taarifa kwa wananchi au viongozi wa juu.

Akizungumza jijini Dodoma leo Novemba 21,2023 hafla ya maadhimisho ya 33 ya kilele cha siku ya Takwimu Afrika
Takwimu Afrika, Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya NBS Dk. Albina Chuwa amesema kuwa takwimu sahihi hupanga program ya maendeleo  hivyo viongozi hao wanapofanya mikutano ni vema wakawa na takwimu hizo sahihi.

Dk. Chuwa ameongeza kuwa haipendezi wananchi kusikia kiongozi anatoa  takwimu ambazo sio sahihi au viongozi kupisha kwenye idadi ya takwimu.

"Tuone umuhimu wa kuzitumia takwimu tukoke kule kwa kukusanya makaratasi tuwe na mfumo wa kisasa wa kidigitali hivyo hata kiongozi anapoenda kijijini ajue kabisa kijiji kina wakazi wangapi, kinachangamoto ya madarasa mangapi, idadi ya matundu ya vyoo vingapi ili kutafuta changamoto zao," amesema Dk. Chuwa.


Kwa Upande wake  mregi rasmi katika kilele hicho Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ameeleza kuwa Takwimu zinasaidia nchi za Afrika kufahamu idadi ya rasilimali watu iliyopo na makundi yake.

Amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotoa Takwimu bora ulimwenguni ambazo zinaaminika si Afrika bali Duniani kwa ujumla.

Ameeleza kuwa  Mwaka 2010 Serikali ilitekeleza mradi wa Mpango kabambe wa Takwimu uliotekelezwa hadi mwaka 2018 na ambao uliimarisha upatikanaji wa Takwimu bora nchini, Nitoe Wito kwa Ofisi ya Mtakwimu msambaze taarifa kwenye Halmashauri zetu kwani Takwimu zinatakiwa kutumiwa kwenye kutafsiri mipango ya maendeleo kwa sekta zote. 

Naye Kamisaa wa Sensa Zanzibar balozi Mohammed Haji Hamza amewapongeza NBS kwa kushirikiana na chuo cha Takwimu Mashariki Afrika kuungana na kushirikiana kuandaa maadhimisho hayo.

"Ni dhahiri ushirikiano huu kati ya Taasisi hizi mbili kuwa ni wamiaka mingi na wengi hawawezi kuona moja kwa moja ushirikiano huo kwani taasisi moja inaiandaa wataalamu na Taasisi nyingine inafaidika na wataalamu hao," ameeleza.



"Kama Kamisaa wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 nimeshuhudia ushiriki na mchango wa wataalmu wa chuo cha takwimu Mashariki mwa afrika katika utekelezaji wa sensa kuanzia awamu ya kwanza hadi tulipokuwa tunandaa  awamu hii ya mwisho ambayo tunatekeleza kwa kweli mchango wa chuo hiki ni mkubwa katika kufanikisha Sensa hii ya mwaka 2022," ameeleza.

Maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika hufanyika Novemba 21 kila mwaka yakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi sahihi ya Takwimu katika mipango ya nchi za Afrika kwani Takwimu zinahitajika wakati wowote.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA): Mchango wa Takwimu Rasmi katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika".


Post a Comment

0 Comments