WIKI YA VISION 2030 YAHITIMISHWA KWA JOGGING YA PAMOJA WASAFI, WIZARA YA MADINI.

 


Na mwandishi wetu


Hatimaye wiki ya Vision  2030, Madini ni Maisha na Utajiri imehitimishwa Novemba 10, 2023 kwa jogging ya pamoja kati ya klabu ya Wasafi Jogging na Madini Sports Club inayoundwa na wafanyakazi wa Wizara ya Madini.

Kwa wiki nzima kuanzia Jumatatu Novemba 6 hadi Ijumaa Novemba 10, 2023, viongozi wa Wizara ya Madini na Watendaji Wakuu wa taasisi zake walipata wasaa wa kuelezea kiundani Mikakati na Mipango yao ya  kutekeleza Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri kupitia kipindi cha runinga na radio cha Good Morning kinachorushwa na Wasafi Media kila asubuhi ya Jumatatu hadi Ijumaa.

Kupitia kipindi hicho kilichokuwa kikirushwa mubashara kutoka viunga vya Wizara na taasisi zake jijini Dodoma, Wizara na Taasisi zake zimeelezea hatua, mikakati na mipango iliyojiwekea kufikia mwaka 2030 kwa kuhakikisha kila Mtanzania wa kawaida anajua ni kwa namna gani Sekta ya Madini inamgusa kwenye maisha yake ya kila siku sambamba na kufungamanisha sekta nyingine ikiwemo ya Kilimo, Maji, Afya pamoja na uchumi kwa ujumla. 

Akizungumzia mazoezi hayo, Mwenyekiti wa Madini Sports Club, John Isangu aliishukuru Wasafi Media kupitia klabu yao ya jogging kwa kusafiri hadi jijini Dodoma na kushiriki mazoezi hayo ya pamoja yenye nia ya kujenga afya pamoja na kutangaza Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri. 

Kwa upande wake, Katibu wa klabu hiyo ya michezo ya Madini, Nuru Kiterebu alisisitiza kuwa michezo ni afya hivyo pamoja na kutekeleza  Vision 2030, Wafanyakazi wa Wizara wanafanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Post a Comment

0 Comments