ZITTO KABWE KUFANYA ZIARA KATIKA MAJIMBO 8 MKOANI KIGOMA KUANZIA NOV 14

 


Taarifa kwa Umma 

KIONGOZI wa chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe,anatarajia kufanya ziara  katika majimbo 8 ya Mkoa wa Kigoma kuanzia Novemba 14 mpaka Disemba 2, 2023. 

Katika ziara hiyo ndugu Zitto atakutana na Viongozi wa matawi 482 (Vijiji 306 na Mitaa 176), Kata 156 ya Majimbo yote 8,Kwa ajili ya  kujadiliana na  Viongozi wa ngazi zote za ACT Wazalendo kuhusu maandalizi na utayari wa chama kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024. 

Pia ndugu Zitto atazungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika Majimbo yote ya Mkoa wa Kigoma. 

Abdallah Khamis

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,Ofisi ya Wasemaji wa Kisekta ACT Wazalendo

Dar es salaam 

Novemba 11, 2023

Post a Comment

0 Comments