Na mwandishi wetu,Karagwe - Kagera.
Waziri wa Ujenzi Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ameungana na Wananchi wa Kata ya Nyakabanga Wilayani Karagwe katika harambee ya kuchangia ujenzi na ukamilishaji wa zahanati ya Kijiji cha Kanogo.
Bashungwa ameongoza harambee hiyo tarehe 20 Aprili 2024 na kufanikiwa kupata kiasi cha jumla ya Shilingi Milioni 46 pamoja na vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na Saruji, Mabati, Tofali, Mchanga, Mawe na Miti.
Wakati akiongoza harambee hiyo, Bashungwa amechangia mabati 400 yatakayotumika kuezeka zahanati hiyo pamoja na kiasi cha shilingi Milioni 10 ambapo awali Ofisi ya Mbunge ilikuwa imeshatoa shilingi Milioni tatu na nusu.
“Pamoja na Milioni tatu na nusu ambazo tayari nimeshachangia, nimeuliza wakati wa kuezeka tunahitaji mabati mangapi, nikaambiwa mabati 380 mimi nitaleta mabati 400 ili tuwe na ziada ya mabati maana yatakatwa na mengine kupigwa misumali vibaya pia nitaongeza Milioni 10 cash”, amesema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Karagwe kuendelea kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kujitoa kuchangia miradi ya maendeleo.
“Zahanati ili ikamilike inahitaji zaidi ya Milioni 80, niwaombe mwananchi muendelee kujitoa ili kufikia mwezi wa nne mwakani tuwe tumekamilisha na huduma zianze kutolewa katika zahanati yetu ya Kanogo”
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nyakabanga, Justine Fidelis ameeleza kuwa ujenzi wa zahanati ulianza kwa nguvu ya wananchi na wadau ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi Milioni 27.8.
0 Comments