BIL. 43 ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI VIPORO

 



Na mwandishi wetu


Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetenga kiasi cha shiligi bilioni 43 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwaajili ya ukamilishwaji wa miradi viporo katika halmashauri zote nchini.


Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Festo Dugange bungeni jijini Dodoma wakati wa maswali na majibu kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mchafu Chakoma aliyetaka kujua lini ujenzi wa wodi za Watoto, Wanawake na Wanaume katika Hospitali ya Wilaya ya Kibaha utakamilika.


Akijibu swali hilo Dkt. Dugange amesema “Katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 43 kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi viporo ya hospitali za Halmashauri. Aidha, majengo yatakayokamilishwa na kuanza kutoa huduma ni pamoja na Wodi za Watoto, Wanawake na Wanaume na kati ya fedha hizo milioni 350 zimetengwa kwaajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kibaha”

Post a Comment

0 Comments