Na mwandishi wetu,Mlimwa Dodoma
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki Iftar iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kwaajili ya watumishi na Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake, Shughuli hiyo imefanyika Mlimwa Jijiji Dodoma na kuhudhuliwa na mamia ya watumishi kutoka Idara, vitengo na Wakuu wa Taasisi mbalimbali zilizoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Viongozi wengine walioshiriki iftar hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mary Maganga.
0 Comments