Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifungua kikao cha kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba Dunia na utatuzi wake, wakati wa Mkutano wa Mwaka 2024 wa Jukwaa la Kibunge la Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani ulioanza leo tarehe 15 Aprili, 2024 katika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Washington DC, nchini Marekani.
Dkt. Tulia amesisitiza umuhimu wa Benki ya Dunia na IMF kuruhusu njia bora zaidi za kusaidia nchi zinazokumbwa na maafa ya mabadiliko ya tabianchi kupitia mfuko wa maafa.
Aidha, ameyaasa Mabunge kuwa chachu ya utekelezaji wa mkataba wa Mazingira wa Paris kwa vitendo zaidi kuliko majadiliano.
0 Comments