JOSEPH BUTIKU AFUNGUKA KUHUSU MUUNGANO,DKT NYONI AWATAJA WANAFUNZI.

 


Na mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) Joseph Butiku ,amesema kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibari watanzania wanatakiwa kujivunia muungano huo na kuacha kuona Muungano huo ni wa viongozi peke yao.


Pia ,Butiku,amewataka vijana nchini kuzidi kujitika katika uzalishaji mali kama njia ya kuulinda muungano huo,


Butiku,ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la kujadili miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibari ambapo Kongamano hilo limeandaliwa na chuo cha ustawi wa jamii.


"Mimi nawaomba vijana na Watanzania kwa ujumla tuuchukulie muungano huu ni wa watanzania wote,tusiuchukulie Muungano ni wa viongozi peke yake"Amesema  Butiku.


Hata hivyo,Butiku amewataka vijana kuhakikisha wanaulinda Muungano kwa kuhakikisha wanajikita katika uzalishaji mali ili nchi zilizo katika Muungano ziache kuwa tegemezi.


Pia Mwanasiasa huyu mkongwe ameonesha matamanio yake kwa atanzania kuacha kuita neno Muungano bali liitwe jina la Tanzania peke yake.


Akizungumzia changamoto za Muungano,Butiku,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutatua changamoto cha Muungano kwa kuhakikisha kunakuwa na tume huru ya uchaguzi.


Kwa upane wake Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,Dkt Jocy Nyomi,amesema nia ya Chuo hicho ya kuandaa Kongamano hilo ni kuwajengea uwezo Wanafunzi hao kuuelewa Muungano ili wao waweze kufahamu kuwa wao ni sehemu ya Muungano.


Aidha,Dkt Nyoni,amesema wao chuo wataendelea kuwafundisha wanafunzi waweze kuufahamu Muungano ili waweze kuulinda.


"Sisi tutaendelea kuwafundisha wanafunzi na kuandaa semina pamoja na warsha mbalimbali ili waweze kuufahamu Muungano na kuweza kuulinda"

Amesema Dkt Nyoni.

Post a Comment

0 Comments