Na mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa amepokea misaada yenye thamani ya Sh 70 milioni kutoka Kampuni ya ASAS na Kampuni ya ORYX kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Misaada hiyo ni mchele tani 10,mafuta Unga tani 10,lita 3,000,unga tani 10 na mitungi ya gesi mikubwa na midogo.
Mchengerwa amepokea misaada hiyo leo April 13,2024 jijini Dar es Salaam huku akiishukuru kampuni hizo kwa msaada huo.
"Kwa niaba ya wananchi wa rufiji tunawashukuru kwa msaada huu ambao tunaamini unakwenda kuwasaidia "Amesema Mchengerwa.
Katika hatua nyingine Mchengerwa amewaelekeza maafisa elimu nchi nzima kuwaelekeza wakuu wote kwenye maeneo yao kuwaangalia wanafunzi hususani katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kuepusha majanga ambayo yanaweza kuwakata wanafunzi.
Pia Waziri huyo ambaye ni mbunge wa rufiji amewaeleke mameneja wa Wakala wa Barabara mjini na vijijini(TARURA) kwenye mikoa mbalimbali kupita kwenye maeneo yalioathirika na mvua na kufanya tasmini ili pindi mvua itakapokamilika ili ujenzi uanze.
Kwa upande Meneja mauzo wa kampuni ORYX ,Shaban Fundi pamoja na Meneta mwendeshaji wa kampuni ya ASAS,Abdalatif Ali,wamesema wameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa ya mafuriko yaliyotokea.
"Kwa niaba ya bodi ya ASAS tumeguswa na majanga yaliyowakuta ndugu zetu na tumeshirikiana na wenzetu wa ORYX kuwatia moyo ndugu. Zetu hawa."
0 Comments