Na mwandishi wetu
Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoani Geita(UVCCM),amesema hatua zinazofanywa za kimaendeleo na Rais wa Jamhuri ya Muungano ,Dkt Samia Suluhu Hassani sio za kubezwa na mtu yoyote bali zinatakiwa kuungwa mkono kutokana na shughuli nyingi za kimaendeleo kuendelea kufanywa ndani ya kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani kuongoza nchi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UVCCM ,Manjale Magambo kwenye kikao na waandishi wa habari Mkoani humu,kikao ambacho kilikuwa na lengo la kuelezea utekelezaji na shughuli za kimaendeleo ambazo zimefanywa na serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais Samia.
Manjale amesema ni ukweli usiopingika Rais Samia amekuwa ni mtekelezaji wa miradi mikubwa ya kimikakati ambayo iliachwa na mtangulizi wake hayati ,Rais Dkt Joseph Pombe Magufuli.ukiwemo ujenzi wa daraja la Busisi Kigongo ambalo kwa sasa lina asilimia 87 za ujenzi wake huku kiasi cha sh,Bilioni mia saba zikiwa zimewekwa kwaajili ya ujenzi.
“Kuna watu wamekua awaoni vitu ambavyo vinafanyika leo hii tumeona hata ndani ya Mkoa wa Geita tumefanya ziara nyingi kwa kuzunguka Mkoa wa Geita,kuna miradi mingi imeanzishwa ikiwemo ya elimu,afya ,Miundo mbinu ya Barabara lakini ukienda pale Chato Hospital ya Kanda ilikuwa ijaanza kufanya kazi lakini ,Mhe Rais alipoingia amesaidia ujenzi wa majengo na kufungua Hospital ya Kanda”Manjale Magambo M/Kiti wa UVVCM Mkoa wa Geita.
Sanjali na hayo Manjale amesema kwenye suala la elimu Serikali ya awamu ya sita imejipambanua kwa kujenga shule maamulum kwaajili ya wasichana ambayo imejengwa kata ya Bomba mbili kwa gharama y ash,Bilioni Tatu.
“Leo hii ukitembelea Mji wa Geita utaona kuna barabara zinajengwa Mhe,Rais ametoa kilomita 17 kwaajili ya kukarabati na kujenga barabara zilizopo kwenye mji wa Geita,Kuna watu wamekuwa na maswali kuhusu ni lini stendi ya Mkoa itajengwa nimekuja na majibu ni kwamba tayari kiasi cha Bilioni 4.4 zimeshatengwa kwaajili ya ujenzi wa stendi ya Kisasa ambayo itaendana na heshima ya Mkoa wetu ambao ni kinara katika uchimbaji wa madini ya dhahabu” Manjale Magambo M/Kiti wa UVVCM Mkoa wa Geita.
Manjale amewataka kuwapuuza wale ambao wamekuwa wakiona hakuna maendeleo yoyote ambayo yamefanywa na kwamba ni vyema wakafanya utafiti kabla ya kutoka adharani na kuanza kumtusi Mhe,Rais Samia Suluhu Hassani.
0 Comments