Na mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya Mbinga *Mhe.Kisare Makori*
leo tarehe 18/04/2024 amekagua mradi wa kituo cha afya, na bweni la shule ya sekondari Mbangamao pamoja ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya Msingi Lusewa iliyopo kata ya ruhuwiko, Ili kuona maendeleo yake na hatua ambazo miradi hiyo imefikia kwasasa.
Aidha, Mhe. Kisare akiwa katika ukaguzi wa miradi hiyo alimshukuru *Mhe.Rais,Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa kutenga fedha nyingi za miradi pamoja na kutoa kiasi cha Tshs 700 M kwa ajili ya vifaa tiba na dawa kwa hospitali, vituo vya afya na zahanati za Halmashauri ya mji Mbinga ili wananchi wapate huduma bora katika mazingira rafiki na karibu zaidi.
Hata hivyo, Alimtaka Mkurugenzi pamoja na wataalamu wake kasoro zote zilizobainishwa na maelekezo yaliyotolewa yafanyiwe kazi ili kukidhi ubora unaokusudiwa, Vilevile alimtaka Mhandisi wa Halmashauri kuhakikisha kila mradi unaotekelezwa anaupitia hatua kwa hatua ili kuepuka kutekeleza chini ya kiwango.
Sambamba na hilo Mhe. Kisare alihaidi kutoa kiasi cha Tshs Laki tano (500,000) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Lusewa kutokana na watoto wa eneo hilo kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kielimu jambo ambalo lina athari kitaaluma.
Mwisho, Mradi wa kituo cha afya Mbangamao umegharimu Tshs Milioni 500 kutoka serikali kuu na mradi umeanza kutoa huduma na ukamilishaji maeneo mengine unaendelea, Bweni la shule ya sekondari umegharimu Tsh 40M na ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi Shule ya Msingi Lusewa Tsh milioni 40.
*Imetolewa na*
*Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbinga*
*April 18, 2024*
0 Comments