SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI IPO MBIONI KUBORESHWA-WAZIRI NDEJEMBI




Na mwandishi wetu

WAZIRI wa nchi,ofisi ya Waziri mkuu (kazi,Ajira,vijana na watu wenye Ulemavu) Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amewahakikishia majaji wa mahakama kuu divisheni ya kazi na wadau wengine Kuwa Serikali inayachukulia kwa uzito mkubwa maoni yao kuhusu kuboresha baadhi ya vifungu vya sheria ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia,kuugua ama kufariki kutokana na kazi.


Mhe.Ndejembi ameyasema hayo wakati wa  Kufunga kikao cha kazi kati ya waheshimiwa mahakama kuu ya divisheni ya kazi kanda ya kati ya magharibi, kamishna wa  kazi,Menejimenti ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi na Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) April 20,2024 mkoani Kigoma.


"Tayari maoni mliyotoa ya kuboresha kifungu Cha 39(2) cha Sheria ya fidia kwa wafanyakazi (sura 263) kilichoweka ukomo wa muda wa kuwasilisha madai bila ya Kutoa wigo wa kupokea madai hayo iwapo Kuna sababu za msingi za kucheleweshwa kwake,tumeshayafanyia kazi na maboresho hayo Kuwa sehemu ya mswada wa maboresho  ya Sheria za hifadhi ya jamii uliosomwa bungeni kwa mara ya kwanza February 2024"amesema Waziri Ndejembi


Aidha Mheshimiwa Ndejembi amesema WCF kwa kushirikiana na kurugenzi ya hifadhi ya jamii,ofisi ya Waziri mkuu (Kazi,Ajira,vijana na watu wenye Ulemavu )wanaendelea na uchambuzi wa maboresho ya Sheria ya fidia kwa wafanyakazi yaliyotolewa na waheshimiwa majaji wa mahakama kuu divisheni ya kazi.








Post a Comment

0 Comments